SOMALIA-USALAMA

Watu watatu wauawa mjini Mogadishu

Watu watatu wamepoteza maisha na wengine tisa kujeruhiwa, baada ya kutokea kwa mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga mjini Mogadishu nchini Somalia.

Askari na polisi wa Somalia wanakagua eneo la mashambulizi Jumamosi, Novemba 6 mjini Mogadishu, shambulizi liliendeshwa na kundi la Al Shabab.
Askari na polisi wa Somalia wanakagua eneo la mashambulizi Jumamosi, Novemba 6 mjini Mogadishu, shambulizi liliendeshwa na kundi la Al Shabab. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Kundi la Al Shabab limesema ndilo lililotekeleza shambulzii hilo lililolenga uwanja wa ndege na Hoteli maarufu inayowapa hifadhi viongozi wa jeshi la AMISOM, na wageni wengine.

Jeshi la AMISOM, linasema mashambulizi hayo yalitokea Mita 200 kutoka lango kuu la uwanja wa ndege, na kuharibu majengo mengine ya watu wa kawaida wanaoshi karibu na uwanja huo wa ndege.

Msemanji wa Al Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab amesema washambulizi wake, walilenga hoteli hiyo ya kifahari ambayo wageni kutoka nchi za nje, hukutana kwa lengo la kuiunga mkono serikali ya Mogadishu.

Shambulizi hili limekuja baada ya wabunge wapya kuapishwa mwishoni mwa mwaka uliopita, wakati huu, wabunge hao wakitarajiwa kumchagua rais.

Kundi la Al Shabab limeendelea kutumia mashambulizi kama haya, kujaribu kuiangusha serikali inayofahamika na kuungwa mkono kimataifa.