LIBYA-SIASA-USALAMA

Mazungumzo yaingia matatani nchini Libya

Khalifa Haftar, mshirika wa karibu wa zamani wa Gaddafi katika miaka ya 1980, akataa kuwepo kwa mazungumzo na serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa
Khalifa Haftar, mshirika wa karibu wa zamani wa Gaddafi katika miaka ya 1980, akataa kuwepo kwa mazungumzo na serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa Reuters/Esam Omran Al-Fetori

Khalifa Haftar, jenerali anayedhibiti mashariki mwa nchi ya Libya, ametangaza kwamba hakuna mazungumzo yaliopangwa kufanyika kati yake na mpinzani wake Fayez Seraj anayeungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Wawili hawa walikuwa walipanga kukutana katika siku zijazo mjini Algiers, kwa mujibu wa chanzo cha karibu cha serikali ya Algeria.

Mazungumzo yao yangejikita kuhusu uwezekano wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Lakini katika mahojiano, jenerali Haftar anasema hakuna mazungumxo yoyote yaliopangwa kufanyika kati yake na Fayez Seraj ambaye anaongoza utawala unaotambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

'' Mazungumzo, ili kuzungumzia demokrasia na uchaguzi, yataanza iwapo watu watu wenye msimamo mkali watashindwa nchini Libya, '' Haftar ameongeza Jumanne hii katika mahojiano na gazeti kutoka Italia la Corriere della Sera.

Kwa mujibu wa jenerali Haftar, hali ya sasa nchini Libya inatoa wito kwa vita badala ya siasa.

Haftar anaona kwamba mazungumzo na Fayez yalianza miaka miwili na nusu iliopita lakini hayakuzaa matunda yoyote.

jenerali Haftar anasema anadhibiti 80% ya ardhi ya Libya.