CAR-MOROCCO-MINUSCA-USALAMA

Askari wa kulinda amani kutoka Morocco wauawa

Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) kinapiga doria mjini Bangui, Septemba 14, 2015.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) kinapiga doria mjini Bangui, Septemba 14, 2015. AFP PHOTO / EDOUARD DROPSY

Nchini Afrika ya Kati, shambulizi lililotokea Jumanne hii mchana iligharimu maisha ya askari wawili wa kulinda amani kutoka Morocco, tume ya Umoja wa Mataifa nchini Afrika ya Kati (Minusca) imetangaza. Katika taarifa yake, Minusca imesema kuwa "askari wengine wawili wamejeruhiwa na wanapata matibabu."

Matangazo ya kibiashara

Askari wa kulinda amani walikuwawakitoa ulinzi kwa msafara wa malori yaliyokua yakibeba mafuta, wakati waliposhambuliwakilomita 60 km magharibi mwa mji wa Obo, kusini-mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kwa mujibu wa Minusca, "watu waliotekeleza shambulio hilo walikimbilia msituni."

Parfait Onanga-Anyanga Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca).
Parfait Onanga-Anyanga Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca). Photo ONU

"Hakuna madai yatakayoeleweka kwa watu wanaoendesha uovu wao dhidi ya askari wa kulinda amani ambao uwepo wao unachangia kurejesha amani na usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati," ameonya Mkuu wa Minusca, Parfait Onanga-Anyanga, ambaye ameahidi kwa "kufanya kila aliwezalo ili waliohusika wa shambulizi hilo wakamatwe."

Hii si mara ya kwanza kwa askari wa kulinda amani kulengwa na machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Mwishoni mwa mwezi Oktoba, maandamano dhidi ya Minusca yalisababisha vifo vya watu wanne na kujeruhi askari wa tano wa kulinda amani. Miezi michache kabla, hasa mwezi Juni, askari wa Umoja wa mataifa aliuawa katika moja ya mitaa ya mjini Bangui Bila hata hivyo wahusika kutambuliwa.