SUDAN-DARFUR

Khartoum: Serikali imekubaliana na makundi mawili ya waasi wa Darfur

Ramani ya eneo la Sudan, Darfur.
Ramani ya eneo la Sudan, Darfur. Reuters/路透社

Serikali ya Sudan imeweka wazi kuwa hivi karibuni wamekubaliani na makundi mawili ya waasi kwenye jimbo la Darfur, kuhusu masuala muhimu baadaya kuwa na vikao visivyo rasmi, huku ikieleza matumaini yake kuwa huenda makubaliano ya mwisho yakafikiwa katika mazungumzo yajayo.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Sudana pamoja na washirika wake, wamekuwa wakipigana na makundi ya wapiganaji wenye silaha kwenye jimbo la Darfur toka mwaka 2003.

Mwezi Agosti mwaka jana, mazungumzo yalifanyika mjini Addis Ababa kati ya Serikali na makundi mawili ya waasi SLM-MM na JEM, mazungumzo yaliyosimamiwa na umoja wa Afrika, yalivunjika baada ya Serikali kutaka waasi hao waeleze maeneo waliyoko.

Toka mwaka jana, rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amekuwa akiratibu mazungumzo hayo jijini Kampala na Addis Ababa, kati ya Serikali ya Sudan na waasi wa SLM-MM na wale wa JEM.

Kufuatia mkutano wake na mwakilishi wa umoja wa Mataifa kwa nchi ya Sudan na Sudan Kusini, Nicholas Haysom Jumatano ya wiki hii, mshauri wa rais Bashir, Ibrahim Mahmoud Hamid alisema Serikali iko kwenye mazungumzo yasiyo rasmi na waasi hao na kwamba wamefikia makubaliano na kwamba wanamatumaini muafaka utafikiwa.

Mshauri huyo alieleza kuwa utawala wa Khartoum umekubaliana na mapendekezo yote yaliyokuwepo katika mkataba wa awali na uratibu umeanza kufanyika na mwakilishi wa Marekani kwa nchi hiyo Donald Booth ambaye nae alisisitiza mkataba huo kutekelezwa.

Serikali ya Sudan imeongeza kuwa, kwa sasa wamewaandikia barua waasi hao kuwaeleza mapendekezo yao na sasa wanasubiri majibu kutoka kwao na kuwaomba kuacha kuwashambulia raia.