DRC-USALAMA

Polisi auawa katika mkoa wa Kasai

Mji wa Tshimbulu unapatikana katika mkoa wa Kasaï ya Kati, nchini DRC.
Mji wa Tshimbulu unapatikana katika mkoa wa Kasaï ya Kati, nchini DRC. RFI

Polisi ameuawa na baadhi ya wafuasi 200 wa kiongozi wa kijadi Kamwina Nsapu, aliyeuawa mwezi Agosti katika shambulizi la mji wa mkoa wa Kasai ya Kati, katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Habari na Msemaji wa serikali Lambert Mende amethibitisha kuwa "jeshi linaendesha operesheni katika eneo hilo dhidi ya raia wasiokua na uzalendo, ambao wanadai kuwa ni wafuasi wa kiongozi wa kijadi Kamwina Nsapu".

Tshimbulu, mji wa kilimo na utawala wenye wakaazi zaidi ya 150,000, unapatikana katika wilaya ya Dibaya, kilomita 120 kusini mwa mji wa Kananga, mji mkuu wamkoa wa Kasai ya Kati, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mwishoni mwa mwezi Septemba, watu wasiopungua 47 waliuawa katika mapigano kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wanaodai kuwa wafuasi wa Kamwina Nsapu katika udhibiti wa uwanja wa ndege wa Kananga.

Kamwina Nsapu aliuawa katika operesheni ya polisi Agosti 12.

Alirejea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo mwezi Aprili baada ya kuishi muda fulani nchini Afrika Kusini.