DRC-UNSC-SIASA

UN yatoa wito kwa utekelezaji wa haraka wa makubaliano ya Disemba 31 DRC

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikaribisha katika tamko la pamoja makubaliano ya Disemba 31, ambayo yatapelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuondokana na mgogoro wa kisiasa unaoendelea (picha ya zamani).
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikaribisha katika tamko la pamoja makubaliano ya Disemba 31, ambayo yatapelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuondokana na mgogoro wa kisiasa unaoendelea (picha ya zamani). REUTERS/Mike Segar

Jumatano hii Januari 4 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikaribisha katika tamko la pamoja makubaliano ya Disemba 31, ambayo yatapelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuondokana na mgogoro wa kisiasa unaoendelea.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya mazungomzo kati ya serikali ya Joseph Kabila na upinzani chini ya upatanishi wa Kanisa Katoliki nchini humo. Makubaliano hayo yatapelekea kuundwa kwa serikali ya mpito kabla ya uchaguzi mpya uliyopangwa kufanyika Desemba 2017. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa utekelezaji wa haraka makubaliano hayo.

Nakala iliandikwa na Ufaransa, ambayo ilikua ikitaka kusaidia kwa hali na mali makubaliano ya Desemba 31 yaliyofikiwa kati ya Maaskofu wa Kanisa katoliki nchini DR Congo na Rais Joseph Kabila. Lakini ili kufikia mwafaka wa pamoja wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Ufaransa inajikita katika ujumbe zaidi kuliko undani wa makubaliano hayo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakaribisha bidi na maelewano ya viongozi wa kisiasa wa DR Congo lakini pia linaomba kwamba bidi hiyo ya viongozi wa kisiasa iendelea "kutatua masuala yote ambayo hayajapatiwa ufumbuzi ikiwa ni pamoja na usimamizi wa pamoja wa uundwaji wa seriklai ya mpito hadi kufanyika kwa uchaguzi mpya Desemba 31. "

Baraza la Usalama la Usalama pia linatoa wito kwa utekelezaji wa makubaliano hayo bila kuchelewa wakati ambapo rais Joseph Kabila bado hajasaini makubaliano yenyewe. "haya ni mafanikio ya kweli," amesema mwakilishi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, François Delattre, ambaye anaamini kwamba kauli hii itaongeza shinikizo ya ziada ili wadau wote katika mgogoro huu wa kisiasa wazingatiye na kutekeleza mkataba huu haraka sana.

Umoja wa Afrika, ambao ulisimamia makubaliano ya kwanza ya tarehe 18 Oktoba 2016, pia umekaribisha makubaliano na kuwataka viongozi wa kisiasa wa DR Congo kuwa na moyo wa uzalendo.