SENEGALI-CHAD-HABRE-SHERIA

Kesi ya rais wa zamani wa Chad kusikilizwa katika mahakama ya rufaa Senegal

Picha ya Hissene Habre, iliopigwa mwaka 1988 wakati wa mkutano kati ya Ufaransa na nchi za Afrika mjini Casablanca.
Picha ya Hissene Habre, iliopigwa mwaka 1988 wakati wa mkutano kati ya Ufaransa na nchi za Afrika mjini Casablanca. FILES / AFP

Kesi ya rais aliyetimuliwa madarakani nchini Chad, Hissene Habre, inasikilizwa Jumatatu, Januari 9 katika mji wa Dakar, nchini Senegal. Na hii itakua ni itakua kesi ya mwisho kwa Hissene Habre kusikilizwa.

Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa mwezi Mei, katika katika mahalama ya mwanzo, rais aliyetawala Chad kati ya mwaka 1982 na 1990 alihukumiwa kifungo cha maisha kwa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, kuwatesa raia na kuwabaka wanawake na wasichana. Kesi hii ya pili pia ni ya mwisho. Hakuna rufaa itakayowezekana baada ya hiyo.

Kwa upande wa wanasheria wa Hissene Habre, wanasema kuna "hoja" isiyoeleweka ambayo inapaswa kubatilisha kifungo cha maisha. Mmoja wa majaji wanne, Diouf Amady kutoka Senegal, hakuwa na umri wa miaka kumi kikazi unaotakiwa kisheria ili ashirikishwe kwa majaji wanaoshughuliki kesi hiyo na hakuwa na uwezo wa kumuhukumu rais wa zamani. "Mahakama ya Rufaa itachukua majukumu yake kwa hoja hii, ambayo ningesema, ilimkandamiza mteja wetu, hojaambayo tuliitaja wakati huo. Ukweli ni kwamba jaji huyo ndiye amebatilisha uamuzi huo uliyoyotolewa na Mahakama , "amesema Mounir Balal.

Hoja "isiyoeleweka", ambayo ingelipatiwa ufumbuzi kabla, wamesema wanasheria wa upande wa mashitaka. "sababu iliyo wazi ni kwamba uteuzi wa jaji huyo ulikuwa kwenye tovuti ya mahakama maalumu ya Afrika kwa miezi kadhaa, wanasheria walizungumzia suala hilo bila mafanikio. Napenda kusema tu kwamba hoja hii haieleweki" amesema kwa upande wake Jacqueline Moudeina, mmoja wa wanasheria wa upande wa mashitaka.

Wanasheria wa Habre watatafuta kuthibitisha kosa jingine la kiutaratibu. Wanaamini kwamba baadhi ya mashahidi, ikiwa ni pamoja na Khadija Hassan Zidane aliyemshutumu Habre kwa kosa la ubakaji, walisema uongo mbele ya mahakama na walishawishiwa na majaji kuzungumzia kosa hilo wakati ambapo walikua walishamaliza kutoa ushahidi wao.

Hatimaye, wanasheria wa upande wa utetezi ambao wanaamini kuwa rais wa zamani wa Chad Hissene Habre alihukumiwa kwa makosa ya uzushi, wataiomba mahkama ya rufaa kutokubali kuwasikiliza kwa mara nyingine tena mashahidi, ikiwa ni pamoja na Saleh Yunus, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa DDS, chombo cha ukandamizaji - lakini pia moja wa washauri katika masuala ya usalama wake wakati huo na ambaye ni rais wa sasa wa Chad, Idriss Déby.

Kesi hii ambayo ilianza kusikilixwa mwaka 2000 iko katika hatua ya mwisho, kwa sababu hakutakuwa na rufaa nyingine kwa Hissene Habre sawa na kwa upoande wa mashitaka.