GAMBIA-MALI

Mali yamtaka raisi Jammeh kuondoka madarakani

Adama Barrow, raisi mteule wa Gambia katikati, akiwa na raisi wa Ufaransa  François Hollande kushoto,na raisi wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta kulia  Mali,14 janvier 2017.
Adama Barrow, raisi mteule wa Gambia katikati, akiwa na raisi wa Ufaransa François Hollande kushoto,na raisi wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta kulia Mali,14 janvier 2017. RFI

Raisi wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ametoa wito wa kumtaka kiongozi wa Gambia Yahya Jammeh kuondoka madarakani mara muda wake utakapokoma ili kuepusha taifa kuingia katika umwagaji damu na kulazimisha uvamizi wa kijeshi.

Matangazo ya kibiashara

Mzozo wa Gambia ulitawala majadiliano katika mkutano ulioandaliwa na ufaransa nchini Mali,ambapo raisi Mteule wa Gambia Adama Barrow alifika kwa kushtukiza na kukutana na viongozi wa Afrika magharibi kutaka usaidizi wa kumaliza mvutano uliopo.

Raisi wa Mali Ibrahim Boubacar Keita aliwaambia wanahabari kuwa mnamo januari 19 nataraji kuona busara za kiafrika zikimshawishi ndugu Jammeh ambaye ni muislamu mwema kuelewa hatima ya Gambia haihiaji umwagaji damu.

Barrow anataraji kuapishwa mnamo January 19 mara utawala wa raisi Jammeh unapofikia ukomo,ingawa kiongozi huyo amekataa kukabidhi madaraka akidai kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Barrow.