Habari RFI-Ki

Drc yakiri tishio la wapiganaji wa zamani M23 kuingia mashariki

Sauti 09:40
Baadhi ya wapiganaji wa zamani wa kundi la M23
Baadhi ya wapiganaji wa zamani wa kundi la M23 AFP PHOTO/ ISAAC KASAMANI

Serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo imesema kuwa waasi wa zamani wa M23 walioko uhamishoni kwa miaka mitatu nchini Uganda wameingia jimboni Kivu kaskazini na kuendesha mashambulizi.Serikali ya jimbo imelitaka jeshi kuimarisha usalama na kuchukua tahadhari,baada ya kuthibitisha kundi la wapiganaji hao wa zamani kuingia Congo wakiwa na silaha ambapo walikamatwa mpakani.