IVORY-COAST

Wanajeshi wengine waingia mtaani kaskazini mwa Ivory Coast

Wanajeshi walioasi wakisalimiana hivi karibuni kwenye mji wa Bouake, Ivory Coast.
Wanajeshi walioasi wakisalimiana hivi karibuni kwenye mji wa Bouake, Ivory Coast. REUTERS/Thierry Gouegnon

Mwanajeshi mmoja wa Ivory Coast aliyeasim ameuawa kaskazini mwa nchi hiyo, wakatik huu vurugu mpya zikishuhudiwa baada ya wanajeshi kuingia mtaani na kuanza kufyatua risasi hewani hali iliyowatisha wananchi.

Matangazo ya kibiashara

Kifo cha mwanajeshi hiyo katika mji wa Yamoussoukro, ni cha kwanza toka wanajeshi hao kuasi wakishinikiza kulipwa marupurupu yao kwenye mji wa Bouake, Januari 5, hali iliyozusha hofu ya usalama.

Hata hivyo vurugu za awali zilizimwa baada ya wanajeshi hao kufikia makubaliano na Serikali juma moja lililopita, na wanajeshi hao walianza kupokea malipo yao Jumanne ya tarehe 17 Januari.

Chini ya makubaliano, wanajeshi hao waliahidiwa kulipwa kiasi cha Franga za Ivpry Coast milioni 12 sawa na dola za Marekani elfu 19 kwa kila mmoja, ingawa bado haijajulikana Serikali itapata wapi fedha za kutekeleza makubaliano haya.

Uasi uliofanywa na wanajeshi hao, ulisababisha mabadiliko makubwa katika ngazi za juu za usalama, mabadiliko ambayo wadadisi wa mambo wanasema ilikuwa ni lazima kwa rais Alassane Ouattara kuyachukua.

Wanajeshi walioasi kwenye mji wa Yamoussoukro hawakujumuishwa kwenye makubaliano ya awali na kwamba mwanajeshi aliyeuawa aliuawa na walinzi wa Serikali nje ya kambi yao.