Shambulizi dhidi ya kambi ya wakimbizi Nigeria: Idadi ya vifo yafikia 70
Imechapishwa:
Idadi ya vifo katika shambulizi dhidi ya kambi ya wakimbizi wa ndani ya rann kaskazini mashariki mwa Nigeria imeongezeka na kufiki 70, huku watu zaidi ya mia moja wakijeruhiwa. Kambi hiyo ilishambuliwa na jeshi la Nigeria.
Jeshi la Nigeria linasema kuwa, lilishambulia kambi iliyokuwa na watu ikifikiri kuwa ni wapiganaji wa Boko Haram, kabla ya kubaini kuwa walikuwa ni raia wa kawaida waliokuwa wanaishi katika kambi hiyo.
Rais wa Nigeria Muhamadu Buhari ameseme amesikitishwa na vifo vya watu zaidi ya 60 walioshambuliwa kimakosa na ndege ya kivita Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Shirika la Msalaba mwekundi linasema wafanyakazi wake sita pia wameuawa katika shambulizi hilo la jeshi.