Hatimaye Yahya Jammeh aondoka nchini Gambia
Imechapishwa: Imehaririwa:
Hatimaye rais aliyemaliza muda wake nchini Gambia Yahya Jammeh ameondoka nchini humo jana Jumamosi baada ya kuitawala nchi hiyo kwa miaka 22
Akiwa ameambatana na rais wa Guinea Alpha Konde, Jammeh aliwapungia mikono wafuasi wake kabla ya kuingia ndani ya ndege isiyokuwa na nembo katika uwanja wa ndege wa Banjul
Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Gambia Jenerali Ousman Badjie ameiambia idhaa ya kiingereza ya rfi kuwa, yuko tayari kufanya kazi na rais mpya Adama Barrow lakini yuko tayari pia kumpisha mtu mwingine
Rais wa Guinea Alpha Conde, na mwenzake wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz walifanya ziara mjini Banjul, nchini Gambia siku ya Ijumaa kwa kujaribu kumshawishi kwa mara ya mwisho Yahya Jammeh ambaye amekubali kuondoka madarakani.
Kwa upande wake, Adama Barrow anatazamiwa kuwahutubia wananchi wa Gambia hivi karibuni kutoka hoteli ya mjini Dakar, nchini Senegal na anasema atarejea Gambia usalama ukiimarika.