AU-KENYA-UONGOZI

Wiki muhimu kwa Umoja wa Afrika kwa kumpata kiongozi mpya

Nkosazana Dlamini Zuma, Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika.
Nkosazana Dlamini Zuma, Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika. AFP/ISSOUF SANOGO

Viongozi wa mataifa ya Afrika, watakutana jijini Addis Ababa nchini Ethiopia mwishoni mwa wiki hii kujadili maswala mbalimbali yanayoligusa bara la Afrika hususan kuhusu usalama na uchumi.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, viongozi hao watakuwa na kazi kubwa ya kumchagua Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja huo kuchukua nafasi ya Nkosazana Dlamini-Zuma kutoka Afrika Kusini.

Wagombea watano wanawania wadhifa huu akiwemo Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Bi Amina Mohammed.

Amina Mohammed, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, aliyependekezwa na Rais Uhuru Kenyatta, kuwania kiti cha uenyekiti wa AU.
Amina Mohammed, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, aliyependekezwa na Rais Uhuru Kenyatta, kuwania kiti cha uenyekiti wa AU. UN Photo/JC McIlwaine

Serikali ya Kenya inasema ina imani kubwa kuwa mgombea wake atashinda, kwa mujibu wa Waziri wa Elimu Fred Matiang'i ambaye amekuwa akiongoza Kamati Maluum ya kumpigia debe Waziri Amina.

Itafahamika kwamba Afrika Mashariki itawakilishwa na Fowsiyo Yusuf Haji Adan, waziri wa zamani wa kigeni nchini Somalia, na Waziri wa sasa wa mambo ya Nje wa Kenya Amina Mohammed, ambaye anapigiwa debe na Rais wake, Uhuru Kenyatta, na kuungwa mkono na rais wa Uganda Yoweri Museveni. Moussa Faki Mahamat, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, ambaye alitangaza kuwania katika kinyang'anyiro hicho katika dakika ya mwisho, ni miongoni mwa wagombea hao.