BURUNDI-DRC

DRC kuwarudisha washukiwa wa uasi 150 nchini Burundi

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza rfi

Washukiwa 150 wa uasi wa Burundi waliokamatwa nchini DRC huenda wakarejeshwa nchini mwao mwaka mmoja baada ya kuzuiliwa katika nchi jirani.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya kushtumiwa kupanga kutekeleza mashambulizi ya kijeshi dhidi ya serikali ya rais Perre Nkurunziza mwaka 2015.

Watu hao walikuwa wanazuiliwa katika tarafa ya Uvira Kusini mwa Jimbo la Kivu mpakani na Burundi huku wengine wakizuiliwa Bukavu mji mkuu wa Mkoa wa Kivu Kusini na wengine jijini Kinshasa.

Duru za kijeshi nchini DRC zinasema kuwa washukiwa hao wa uasi hawatakiwi tena kuishi nchini humo.

Raia hao wa Burundi wamekuwa wakisema kuwa wao ni wakimbizi waliokimbia DRC wala sio waasi kama inavyodaiwa na serikali ya Bujumbura.

Nalo Shirika la Umoja wa Mataifa ambalo lina jeshi la kulinda amani nchini humo MONUSCO, linasema halijashirikishwa katika mpango huo ambao wanasema huenda ukahatarisha maisha ya raia hao wa Burundi ikiwa watarudishwa nyumbani.