LIBYA-USALAMA

Vikosi vya Libya vyatangaza kudhibiti robo ya mji wa Benghazi

Vikosi vya mashariki mwa Libya vimetangaza Jumatano wiki hii kudhibiti karibu eneo nzima lililokua likikabiliwa na mapambano ya kwa muda mrefu katika mji wa Benghazi.

Askari watiifu kwa serikali ya Libya inayotambuliwa wakisherehekea kudhibitiwa kwa ngome kuu ya wapiganaji wa kijihadi katika mji wa Benghazi Februari 23, 2016.
Askari watiifu kwa serikali ya Libya inayotambuliwa wakisherehekea kudhibitiwa kwa ngome kuu ya wapiganaji wa kijihadi katika mji wa Benghazi Februari 23, 2016. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Kama taarifa hii itathibitishwa, kutekwa kwa mji wa Ganfouda itakuwa mafanikio makubwa kwa jeshi la kitaifa la Libya, ambalo linapambana kwa zaidi ya miaka miwili na makundi ya wanamgambo wa Kiislam katika mji mkuu wa mashariki mwa Libya.

"Mji wa Ganfouda uko chini ya himaya ya Majeshi yetu," Msemaji wa vikosi vya Mashariki, Ahmed al Mismari ameliambia shirika la Reuters.

Wapiganaji sitini na mbili wamekamatwa, lakini familia 30 na wafanyakazi 46 wa kigeni wamekombolewa, amesema msemaji mwingine wa vikosi vya Mahariki mwa Libya.