GAMBIA-BARROW-ECOWAS

Rais Barrow arejea nchini Gambia wiki moja baada ya kuapishwa

Rais mpya wa gambia, Adama Barrow, atazamiwa kurejea nchini mwake, siku 15 baada ya kuhamishwa nchini Senegal.
Rais mpya wa gambia, Adama Barrow, atazamiwa kurejea nchini mwake, siku 15 baada ya kuhamishwa nchini Senegal. REUTERS/ Thierry Gouegno

Rais wa Gambia Adama Barrow anatazamiwa kurejea leo Alhamisi nchini Gambia, huku wananchi wengi wakisubiri kurejea kwake toka kuapishwa kwake wiki moja iliyopita mjini Dakar, nchini Senegal baada ya kuondoka kwa Yahya Jammeh Januari 21.

Matangazo ya kibiashara

Bw Barrow alipokelewa nchini Senegal tangu Januari 15 kufuatia ombi la Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS), ambayo ilikua ikihofia usalama wake endapo BwJammeh atakua bado madarakani. Adama Barrow alikua amepinga kurejea nchini Gambia wakati huu akihofia usalam wake.

Gambia, taifa dogo linalozungumza Kiingereza linazungukwa na Senegal, isipokuwa eneo dogo la pwani ambako watalii wengi hutembelea, iliongozwa kwa mkono wa chuma kwa miaka 22 na Yahya Jammeh, mwanajeshi wa zamani.

Rais Adama Barrow ametangaza kurejea nchini Gambia Alhamisii (saa 10:00 saa za kimataifa) kwenye ukurasa wake wa Facebook. Hata hivyo kurejea kwake nchini Gambia kumethibitishwa na chanzo cha Ofisi ya rais wa Senegal, na baadaye washirika wa karibu wa rais wa Senegal na Gambia.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika Afrika Magharibi, Mohamed Ibn Chambas, ambaye aliarifu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali hiyo katika kikao cha faragha,ataongozana na Bw Barrow Alhamisi hii kutoka Dakar kwenda Banjul, kwa mujibu wa chanzo cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.