GAMBIA-ECOWAS-USHIRIKIANO

Rais wa Gambia ataka jeshi la ECOWAS kubaki nchini mwake

Askari wa kikosi cha ECOWAS, kiliotumwa katika mji wa Gambia, Banjul, Januari 23, 2017.
Askari wa kikosi cha ECOWAS, kiliotumwa katika mji wa Gambia, Banjul, Januari 23, 2017. REUTERS/Thierry Gouegnon

Rais mpya wa Gambia Adama Barrow ameomba jeshi la muungano wa nchi za Afrika Magharibi ECOWAS kusalia nchini mwake kwa muda wa miezi sita.

Matangazo ya kibiashara

Ombi hili la Barrow limekuja wakati huu akitarajiwa kurudi nyumbani akitokea jijini Dakar nchini Senegal.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Magharibi wa Afrika Mohammed Ibn Chambas, amesema ombi hilo la rais Barrow liko mikononi mwa viongozi wa ECOWAS ili kuamua.

Bw Barrow alipokelewa nchini Senegal tangu Januari 15 kufuatia ombi la Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS), ambayo ilikua ikihofia usalama wake endapo BwJammeh atakua bado madarakani. Adama Barrow alikua amepinga kurejea nchini Gambia wakati huu akihofia usalam wake.

Gambia, taifa dogo linalozungumza Kiingereza linazungukwa na Senegal, isipokuwa eneo dogo la pwani ambako watalii wengi hutembelea, iliongozwa kwa mkono wa chuma kwa miaka 22 na Yahya Jammeh, mwanajeshi wa zamani.

Rais Adama Barrow ametangaza kurejea nchini Gambia Alhamisii (saa 10:00 saa za kimataifa) kwenye ukurasa wake wa Facebook. Hata hivyo kurejea kwake nchini Gambia kumethibitishwa na chanzo cha Ofisi ya rais wa Senegal, na baadaye washirika wa karibu wa rais wa Senegal na Gambia.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika Afrika Magharibi, Mohamed Ibn Chambas, ambaye aliarifu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali hiyo katika kikao cha faragha,ataongozana na Bw Barrow Alhamisi hii kutoka Dakar kwenda Banjul, kwa mujibu wa chanzo cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.