SOMALIA-UCHAGUZI

Uchaguzi wa urais nchini Somalia kufanyika tarehe 8 mwezi Februari

Uchaguzi wa urais nchini Somalia umepangwa kufanyika tarehe 8 mwezi Februari.

Mzee akisaidiwa kupiga kura kuwachagua wabunge katika jimbo la  Baidoa mwaka 2016
Mzee akisaidiwa kupiga kura kuwachagua wabunge katika jimbo la Baidoa mwaka 2016 Simon Maina/AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili limetolewa na Tume ya Uchaguzi nchini humo baada ya zoezi hili kuahirishwa kwa miezi kadhaa kutokana na hali ya kiusalama nchini humo.

Tume hiyo imesema wale wanaotaka kuchaguliwa katika nafasi hiyo wana hadi tarehe 29 mwezi Januari kuwasilisha maombi yao.

Rais Hassan Sheikh Mohamud mwenye umri wa miaka 61 anatarajiwa kutetea wadhifa wake katika uchaguzi huu.

Wagombea wengine ni pamoja na Omar Abdirashid Ali Sharmarke, rais wa zamani Sheik Sharif Ahmed, Mohammed Abdullahi Mohamed, Ali Haji Warsame na mwanamke wa pekee Fadumo Dayib.

Uchaguzi huu utafanyika miezi sita baada ya mara ya kwanza kupangwa kufanyika mwezi Agosti mwaka uliopita.

Ucheweleshwaji wa Uchaguzi huu baada ya kuwepo kwa mzozo kati ya koo mbalimbali kuhusu Uchaguzi wa wabunge.

Wabunge 275 ndio watakaomchagua rais katika Uchaguzi huo.