RFI-UFARANSA-MALI

FMM yataka sheria ifuate mkondo wake kuhusu mauaji ya Dupont na Verlon nchini Mali

Ghislaine Dupont na Claude Verlon, Julai 30, 2013 katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Mali.
Ghislaine Dupont na Claude Verlon, Julai 30, 2013 katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Mali. RFI/Pierre René-Worms

Katika hali ya kuendelea kutafuta ushahidi kuhusu mauaji ya waandishi wawaili wa RFI Ghislaine Dupont na Claude Verlon waliouawa nchini Mali, RFI imepongeza baadhi ya vituo ambavyo vimekua vikizungumzia mauaji hayo.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kupeperushwa kwa kipindi maalum kilichopewa jina la Special Envoy katika kituo cha Televisheni cha Ufransa cha France 2 na kupewa jina la Mahabusu wa taifa, uongozi wa RFI umepongeza kituo kingine kwa kuendeleza uchunguzi dhidi ya kifo cha waandishi wa habari wawili wa RFI Ghislaine Dupont na Claude Verlon waliouawa Novemba 2 mwaka 2013 mjini Kidal, kaskazini mwa Mali na waasi.

Ghislaine Dupont na Claude Verlon walikuwa katika mji a Kidal mwezi Novemba 2013 kwa ajili ya maandalizi ya siku maalum iliyopangwa kwa vituo vya RFI katika mkesha wa ufunguzi wa "mazungumzo ya makundi mbalimbali nchini Mali" na uchaguzi wa wabunge nchini humo. Baada ya kuachiwa huru kwa mateka wa Arlit, tarehe 29 mwezi Oktoba mwaka 2012, wakati ambapo walikua walifika katika mji wa Kidal, walizungumzia tukio hilo wakiwa na wakalimani wao katika mji huo.

Baadhi ya ushahidi na vielelezo vya France 2 vinabainisha uhusiano kati ya operesheni iliyopelekea kuachiliwa huru kwa mateka wa Arlit na mauaji ya waandishi wa habari wawili wa RFI. Makala haya pia yanaonyesha kuwa kuna vitu ambavyo viliwekwakwenye kompyuta binafsi ya Ghislaine Dupont.

FMM inataka mahakama kutimia ushahidi huo na kuwatuma wanasheria wake ili wamuombe afisa anayeshughulikia kesi hiyo kuendelea na uchunguzi.

Uongozi wa FMM unaomba haki itendeke ili ukweli ujulikane kuhusu mauaji ya Ghislaine Dupont na Claude Verlon na wahusika wakamatwe, wahukumiwe.

Mkurugenzi wa RFI Cecile Megie ameomba ukweli uwekwe wazi ili wahusika wakamatwe na kuadhibiwa.