AU-UONGOZI

AU yamchagua kiongozi mpya

Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad,  Moussa Faki Mahamat achaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika..
Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, Moussa Faki Mahamat achaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika.. AFP PHOTO / FETHI BELAID

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Chad Moussa Faki amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa tume ya ya Umoja wa Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Mshindani, mkuu wa bwana Faki katika duru ya mwisho ya upigaji kura, alikuwa ni waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Kenya Amina Mohamed. Zoezi hilo la upigaji kura lilifanyika wakati wa kikao cha Umoja wa Afrika (AU) mjiji Addis Ababa, nchini Ethiopia.
Faki anachukua nafasi ya Dlamini Zuma kutoka Afrika Kusini ambaye kipindi chake cha kuhudumu kimemalizika.

Wagombea watano waliokuwa wakiwania wadhifa huo ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Moussa Faki Mahamat, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Amina Mohammed, Abdoulaye Bathily ,mwanadiplomasia kutoka Senegal, aliyekuwa mshauri wa rais wa Equatorial Guinea Mba Mokuy na mwanasiasa mkongwe kutoka Botswana Pelonomi Venson-Moitoi.

Wakati huo huo rais wa Guinea-Conakry Alpha Conde amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika.

Conde mwenye umri wa miaka 78 anachukua nafasi ya rais wa Chad Idriss Derby ambaye amemaliza muda wake wa kuongoza Umoja huo kwa muda wa mwaka moja.