DRC-M23-USALAMA

Helikopta mbili za jeshi la DR Congo zaanguka

wapiganaji wa kundi la zamani la M23, Februari 2014.
wapiganaji wa kundi la zamani la M23, Februari 2014. AFP PHOTO/ ISAAC KASAMANI

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imethibitisha kuanguka kwa ndege mbili za kijeshi Mashariki mwa nchi hiyo, zikiwa na wanajeshi wanne.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali Lambert Mende ameliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa, haijafahamka ni kitu gani kilichosababisha kuanguka kwa ndege hizo karibu na mpaka wa Rwanda na Burundi.

Duru zinasema kuwa ndege hizo zilianguka wakati zinawashambulia waasi wa zamani wa M 23.

Wapiganaji 30 wa M23 wakimbilia nchini Rwanda

Jeshi la Rwanda limetangaza katika taarifa yake kwamba wapiganaji thelathini wa kundi la zamani la waasi wa DR Congo la M23 wameingia nchini Rwanda wakikimbia mashambulizi ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Watu hawa thelathini walivuka mpaka Jumapili Januari 29, wakitokea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Kwa mujibu wa serikali ya Rwanda ambayo imekamata, watu hao wanasema kuwa ni wapiganaji wa M23 waliokimbia mashambulizi ya jeshi la DR Congo.

Serikali ya Kigali imehakikisha kwamba baadhi ya wapiganaji hao wamehudumiwa na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu kulingana na sheria ya kimataifa ya kibinadamu.

Katika wiki za hivi karibuni, waasi wa zamani wa kundi la M23 wamekua wakionekana katika maeno mbalimbali ya ukanda huo.

Januari 19, serikali ya Uganda ilikubali kuwa haitambui waliko wapiganaji arobaini wa kundi la zamani la waasi la M23.

Watu hao walitoroka kutoka eneo ambapo walikuwa wlikusanywa kwa miaka mitatu.