MORROCO-AU

Morocco yakubaliwa kujiunga upya na AU

Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika wamemua Jumatatu wiki hii kuikubalia Morocco kujiunga upya na Umoja wa Afrika. Wakati huo huo Tume ya Umoja wa Afrika imempata kiongozi mpya, huku rais wa Guinea, Alpha Condé, alkichaguliwa kuwa rais wa Umoja wa Afrika

Mfalme Mohammed VI, ambaye alishiriki kikao cha Umoja wa Afrika Jumatatu wiki hii mjini Addis Ababa, alifanya ziara nyingi za kikazi katika miji mikuu ya nchi za Afrika ili kupata uungwaji mkono.
Mfalme Mohammed VI, ambaye alishiriki kikao cha Umoja wa Afrika Jumatatu wiki hii mjini Addis Ababa, alifanya ziara nyingi za kikazi katika miji mikuu ya nchi za Afrika ili kupata uungwaji mkono. REUTERS/Maghreb Agence Press/Pool
Matangazo ya kibiashara

Angalau Marais na viongozi wa serikali 39 kati ya 54 wanachama wa Umoja wa afrika wamepiga kura ya ndio kwa Morocco kujiunga upya na AU, kwa mujibu wa rais wa Senegal Macky Sall, ambaye ameshiriki katika zoezi la kuchunguza faili ya Morocco Jumatatu wiki hii mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia.

Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, amethibitisha kuwa "nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Afrika walibaliwa ombi la Morocco kurejea katika Umoja wa Afrika."

Mwaka 1984, Morocco ilijiondoa katika Muungano wa Umoja wa Afrika wa zamani (OAU) ambao ulibadili jina na kuwa Umoja wa Afrika (AU) katika miaka ya 2000, kwa kupinga kutambuliwa kwa eneo la Shara Magharibi kama taifa huru.

Wakati huo OAU ilikubali Jamhuri ya Kiarabu Sahara kama taifa huru. Eneo hili lilitangazwa na kundi la Polisario Front wakati ambapo serikali y Rabat ilikua ikichukulia eneo hili kama sehemu yake.

Morocco imetangaza mwezi Julai mwaka jana nia yake ya kurudi AU.

Mfalme Mohammed VI, ambaye alishiriki kikao cha Umoja wa Afrika Jumatatu wiki hii mjini Addis Ababa, alifanya ziara nyingi za kikazi katika miji mikuu ya nchi za Afrika ili kupata uungwaji mkono.

Jumatatu, siku ya kwanza ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Moussa Faki Mahamat, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, kuchukua nafasi ya Nkosazana Dlamini-Zuma, kutoka Afrika Kusini kwa kipindi cha miaka minne.

Mkuu wa Nchi ya Guinea, Alpha Condé, alichaguliwa kuwa rais wa Umoja wa Afrika.