Habari RFI-Ki

Hatimaye Morocco yakubaliwa kujiunga katika Umoja wa Afrika AU

Sauti 09:44
Mfalme wa sita wa Morocco, Mohamed akiwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, Ikulu, Dar es Salaam, 24 October 2016.
Mfalme wa sita wa Morocco, Mohamed akiwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, Ikulu, Dar es Salaam, 24 October 2016. Ikulu/Tanzania/issa Michuzi

Hatimaye Morocco imekubaliwa kujiunga na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.Marais na viongozi wa serikali 39 kati ya 54 wanachama wa Umoja wa afrika walipiga kura ya ndio kwa Morocco kujiunga upya na AU huku wengine wakisusa.Morocco ilijiondoa kwenye umoja wa Afrika miaka 30 iliyopita baada ya umoja huo kulitambua eneo la Sahara magharibi kama eneo huru.