CHAD-ELIMU

Wanafunzi wachoma shahada zao nchini Chad

Moja ya maeno ya muhimu mjini N'Djamena
Moja ya maeno ya muhimu mjini N'Djamena PHILIPPE DESMAZES / AFP

Kwa ishara hii wanafunzi walitaka kusikilizwa na kuandamana dhidi ya kukosekana kwa ajira nchini Chad.

Matangazo ya kibiashara

Moussokdjim Berodjingar, ambaye ni kiongozi kundi la wanafunzi waliochoma shahada zao amesema wamefanya hivyo baada ya kukaa miaka mingi bila kupata ajira.

'' Nchini Chad kupatikana kwa ajira katika sekta binafsi si rahisi kutokana na ukosefu wa viwanda '' Moussokdjim Berodjingar ameiambia BBC Afrique.

'' Vijana waliomaliza shule kwametelekezwa na hatma yao kwa sasa haijulikani '' Bw Berodjingar ameongeza.

Moussokdjim Berodjingar amesema hata yeye mwenyewe ameamua kuchomwa shahada yake ya chuo kikuu katika fasihi ya kisasa.

Shahada tulizokua nazokwa muda mrefu ni kama karatasi tu , hazina maana yoyote, wala haziwezi kutupatishia kazi, '' Bw Berodjingar amelaumu.

Baadhi ya wanafunzi waliomaliza shule wana zaidi ya miaka 10 wakitafuta kazi lakini hawapati.

'' Hakuna fedha kw ujenzi wa makampuni, mabenki yanatoa mikopo kwa wafanyakazi tu, kwa wale wenye kuwa na dhamana.

Mtoto wa maskini hana nafasi katika ulimwengu huu, na tayari amekatta tamaa, '' amebaini Berodjingar.

Benki kuu ya mjini Ndjamena, Chad.
Benki kuu ya mjini Ndjamena, Chad. Wikimedia Commons/Notrchad