Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA-SIASA

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma afananishwa na Trump

Gazeti la Mail and Guardian lamfananisha rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na Trump
Gazeti la Mail and Guardian lamfananisha rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na Trump REUTERS/Philimon Bulawayo

Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, imejibu kwa hasira baada ya gazeti la The mail and Guardian kuchapisha makala inayomfananisha na rais wa Marekani Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

Gazeti la Mail na Guardian limechapisha makala yenye kichwa cha habari "Trump na Zuma wabaya zaidi kuliko waongo."

Ofisi ya Rais inaona kuwa makala hiyo imechapishwa kinyume na "mikataba ya uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza."

Bunge la Afrika Kusini linafikiria kupendekeza sheria inayoadhibu lugha ya chuki kwa viongozi wa nchi. Matusi kwa rais bila shaka itakua ni uhalifu.

Ikumbukwe kwamba Rais Jacob Zuma anakabiliwa na kampeni kadhaa za kumchafua tangu kashfa iliyoitwa "Nkandla" iibuke.

Rais Zuma anashtumiwa hasaa katika chama chake cha ANC, chama tawala nchini Afrika Kusini.

Rais wa Afrika Kusini alipatikana na hatia ya kuwa alitumia Euro milioni 20 ya hazina ya Afrika Kusinikwa kujenga makazi yake binafsi katika eneo la Nkandla.

Alitakiwa kulipa sehemu ya fedha ya fedha hizo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.