CAMEROON-RFI-ABBA

Kesi ya mwanahabari wa idhaa ya Kihausa ya RFI yaahirishwa tena

Mwanahabari wa Idhaa ya Kihausa ya RFI Ahmed Abba azuiliwa nchini Cameroon kwa shutma za ugaidi.
Mwanahabari wa Idhaa ya Kihausa ya RFI Ahmed Abba azuiliwa nchini Cameroon kwa shutma za ugaidi. facebook

Kesi ya ugaidi dhidi ya mwanahabari wa RFI Hausa nchini Nigeria Ahmed Abba, imeahirishwa tena na Mahakama ya kijeshi nchini Cameroon.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya Mahakama hiyo kukataa ripoti ya watalaam wa ugaidi, waliojaribu kuishawishi Mahakama kumpata Abba na makosa hayo.

Abba amekuwa akizuiliwa kwa zaidi ya mwaka mmoja baada ya kukamatwa nchini Cameroon kwa madai hao, huku Mahakama na viongozi wa mashtaka wakishindwa kutoa ushahidi wa kumfungulia mashtaka.

Uongozi wa RFI na mashirika ya wanahabari ulimwenguni wanaendelea kushinikiza kuachiliwa kwa mwanahabari huyo.