MALI-USALAMA-SIASA

Wiki yenye maamuzi katika utekelezaji wa mkataba wa amani nchini Mali

Kusainiwa rasmi kwa mkataba wa Amani, mjini Bamako, Mei 15, 2015 (picha ya zamani).
Kusainiwa rasmi kwa mkataba wa Amani, mjini Bamako, Mei 15, 2015 (picha ya zamani). AFP PHOTO / HABIBOU KOUYATE

Baada ya makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa ngazi ya juu uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Bamako, nchini Mali, na tayari kuna ulazima sasa kukuingi katika hatua muhimu. Haijafahamika iwapo ni ratiba mpya au maendeleo zaidi katika utekelezaji wa makubaliano. Wiki hii una ulazima maamuzi yachukuliwe.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya mkutano huo, kundi la waasi la Azawad na makundi mengine washirika yamekua yakitoa hotuba ambazo zinapongeza makubaliano hayo. Kuna maendeleo muhimu katika mikataba hii mipya. mazungumzo yalianza kati ya pande husika na pakua na maendeleo. Lakini kama masharti mapya hayatatekelezwa itakuwa tu kama "ahadi".

Katika suala la ahadi mpya hivyo ni pamoja na kuwekwa kwa viongozi wa mpito, ambao wanatakiwa kurejesha utawala kaskazini mwa Mali. Wiki hii, viongozi hao watawekwa katika majimbo ya Gao na Timbuktu, hayo ni baadhi ya mambo yaliyopangwa kufanyika wiki hii. Wiki ijayo, doria ya pamoja inapaswa kuanza kwa kuyashirikisha makundi ya waasi yaliosaini mkataba wa amani na askari wa jeshi la serikali.

Lakini maswali mengi bado yanaendelea kujitokeza. Kwanza, bado hayajajulikana majina ya wawakilishi wa viongozi hawa wa mpito. Ni serikali ambayo itapendekeza majina ya watu watakaoongoza majimbo hayo.