NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Mkutano wa wafadhili kwa waathirika wa Boko Haram wafanyika

Mashirika yasio ya kiserikali na nchi wafadhili wanaokutana tangu Alhamisi wiki hii katika mji wa Oslo wanatazamiwa kujaribu kuongeza msaada wa kibinadamu wa dharura kwa mamilioni ya wakimbizi wa ndani wa "migogoro iliyosahaulika" duniani.

Familia za wakimbizi waliolazimika kuyahama makaazi yao kutokana na vurugu za Boko Haram, Februari 14, 2017 katika jombo la Borno nchini Nigeria.
Familia za wakimbizi waliolazimika kuyahama makaazi yao kutokana na vurugu za Boko Haram, Februari 14, 2017 katika jombo la Borno nchini Nigeria. AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakimbizi hao wanakabiliwa na njaa kaskazini mashariki mwa Nigeria ambapo wanajihadi wa kundi la Boko Haram wanaendelea na harakati zao.

Lengo la Umoja wa Mataifa ni kuchangisha kwa muda wa siku mbili Alhamisi na Ijumaa katika mji mkuu wa Norway Euro bilioni 1.4 ya ahadi kwa ukanda wa Ziwa Chad, unaundwa na Nigeria, Niger, Cameroon na Chad.

Ukanda huo ambao kwa sasa unakabiliwa na ukame umeendelea kuathirika na vurugu kwa kipindi cha miaka nane sasa. Shughuli mbalimbali katika shule, zahanati na kilimo vimesimama. Kwa miguu na bila rasilimali yoyote, raia wamelazimika kuwakimbia wapiganaji wa Boko Haram.

Wakati huo huo upungufu wa chakula umefikia viwango vya kutisha, huku watu milioni 5.1 wakikosa chakula na zaidi ya watoto 500,000 wakisumbuliwa na utapiamlo sugu.

Waziri Mkuu wa Norway Børge Brende, akifungua mkutano wa asasi za kiraia Alhamisi hii, alizungumzia "migogoro iliyosahaulika" duniani.