Waandamanaji nchini Nigeria waomba raia wa Afrika Kusini kufukuzwa

Waandamanaji waliandamana Alhamisi Nigeria wakiomba kufukuzwa kwa raia wa Afrika Kusini waishio nchini Nigeria wakilipiza kisasi kile kinachotokea nchini Afrika Kusini, Februari 23, 2017.
Waandamanaji waliandamana Alhamisi Nigeria wakiomba kufukuzwa kwa raia wa Afrika Kusini waishio nchini Nigeria wakilipiza kisasi kile kinachotokea nchini Afrika Kusini, Februari 23, 2017. REUTERS/Afolabi Sotunde

Nchini Nigeria maelfu ya watu waliingia mitaani Alhamisi hii Februari 23 wakidai kufukuzwa kwa raia wa Afrika Kusini baada ya vurugu na mateso walioyapata raia wa Nigeria waishio nchini Afrika Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa Abuja, makao makuu ya kampuni ya simu kutoka Afrika Kusini ya MTN yaliharibiwa na waandamanaji.

Shirikisho la wanafunzi wa Nigeria walitoa masaa 48 kwa raia wa Afrika Kusini waishio nchini Nigeria kuondoka nchini humo, na kutishia kuimarisha maandamano yao na kushambulia makampuni mengine kutoka Afrika Kusini.

Ongezeko hili la mashambulizi dhidi ya wageni ni kufuatia visa vya uporaji vilivyoshuhudiwa wiki hii ambapo maduka yasiyopungua 20 yanayomilikiwa na raia wa Nigeria nchini Afrika Kusini yalishambuliwa.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini, Malusi Gigaba, ghasia za kibaguzi zimshika kasi mwaka huu na maandamano dhidi ya wahamiaji yamepangwa kufanyika Ijumaa wiki hii mjini Pretoria.