GAMBIA-SENEGAL-USHIRIKIANO

Rais wa Gambia afanya ziara ya kiserikali mjini Dakar

Rais wa Gambia Adama barrow na mwezake wa Senegal Macky Sall wakisubiri kusaini mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia siku ya Jumamosi.
Rais wa Gambia Adama barrow na mwezake wa Senegal Macky Sall wakisubiri kusaini mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia siku ya Jumamosi. © Getty Images

Rais wa Gambia Adama Barrow amefanya ziara ya kiserikali nchini Senegal Alhamisi wiki hii, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano kwenye Ofisi ya rais wa Senegal Hamidou Elhadji Kassé.

Matangazo ya kibiashara

Bw Barrow aliwasili mjini Dakar Alhamisi wiki hii saa 4:00 asubuhi (saa za Afrika Magharibi).

Rais wa Gambia Adama Barrow alikutana kwa mazungumzo na mwenzake wa Senegal Macky Sall Alhamisi mchana.

Kwa mujibu wa Ofisi ya rais wa Senegal, Bw Barrow atafanya ziara binafsi Ijumaa kwa viongozi wa kidini.

Mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia itasainiwa siku ya Jumamosi.

Adama Barrow alichaguliwa kuwa rais wa Gambia tarehe 1 Desemba 2015, lakini mtangulizi wake Yahya Jammeh alikataa kuondoka madarakani baada ya kukubali awali kushindwa.

Bw Barrow hatimaye aliapishwa kwenye ubalozi wa Gambia mjini Dakar Januari 19 baada ya Yhya Jammeh kukataa kuondoka madarakani licha ya upatanishi wa ECOWAS.

Tarehe 20 Januari, Jammeh hatimaye alikubali kuachia ngazi baada ya ECOWAS kutishia kuingilia kijeshi nchini Senegali.

Macky Sall, rais wa Senegal, alikuwa mgeni rasmi wa Siku ya Uhuru wa Gambia tarehe 18 Februari.