RFI-AHMEDA ABBA-CAMEROON

Kesi ya mwanahabari Ahmed Abba yaahirishwa

Mwanahabari wa RFI, idhaa ya Hausa ya Nigeria, Ahmed Abba, ambaye anashikiliwa nchini Cameroon.
Mwanahabari wa RFI, idhaa ya Hausa ya Nigeria, Ahmed Abba, ambaye anashikiliwa nchini Cameroon. via facebook profile

Kesi ya ugaidi dhidi ya mwanahabari wa RFI Idhaa ya Hausa nchini Nigeria Ahmed Abba, imeahirishwa tena na Mahakama ya kijeshi nchini Cameroon.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya Mahakama hiyo kukataa ripoti ya watalaam wa ugaidi, waliojaribu kuishawishi Mahakama kumpata Abba na makosa hayo.

Kesi hii imepangwa kusikilizwa tena ifikapo marchi24 mwaka huu,

Abba amekuwa akizuiliwa kwa zaidi ya mwaka mmoja baada ya kukamatwa nchini Cameroon kwa madai hayo, huku Mahakama na viongozi wa mashtaka wakishindwa kutoa ushahidi wa kumfungulia mashtaka.

Uongozi wa RFI na mashirika ya wanahabari ulimwenguni wanaendelea kushinikiza kuachiliwa kwa mwanahabari huyo.