ZIMBABWE-MUGABE-AFYA

Mugabe asafiri Singapore kuchunguza hali ya afya yake

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akisoma kadi ya kuzaliwa wakati wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa mjini Harare, Februari 21, 2017.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akisoma kadi ya kuzaliwa wakati wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa mjini Harare, Februari 21, 2017. REUTERS/Philimon Bulawayo

Rais wa Zimabwe Robert Mugabe amesafiri kwenda nchini Singapore kuangalia hali yake ya kiafya baada ya kusherehekea umri wa miaka 93.

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni, afya ya rais Mugabe imeonekana kudorora na hata kupata matatizo ya kutembea.

Msemaji wake amesema kiongozi huyo ambaye ametangaza kuwa atawania urais mwaka ujao, atarejea jijini Harare mapema wiki ijayo.

Hayo yakijiri Mahakama kuu nchini Zimbabwe imepiga marufuku walimu katika shule za msingi kuwapa wanafunzi dhabu ya viboko.

Marufuku haya pia yatatekelezwa hadi nyumbani kwa kile Mahakama inasema ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

Hatua hii imekuja baada ya mzazi mmoja kwenda Mahakamani kutaka Mahakama kufanya uamuzi baada ya mwanfunzi wa darasa la kwanza kupigwa viboko baada ya kazi yake ya ziada kutotiwa saini.