ICC-AFRIKA

Silvia Fernández: ICC haiwalengi viongozi wa Afrika

Rais wa ICC, Silvia Fernandez de Gurmendi, hivi karibuni alitembelea Uganda kupata taarifa kuhusu fedha zitazopewa waathirika wa ICC.
Rais wa ICC, Silvia Fernandez de Gurmendi, hivi karibuni alitembelea Uganda kupata taarifa kuhusu fedha zitazopewa waathirika wa ICC. AFP PHOTO / POOL / MICHAEL KOOREN

Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC Jaji Silvia Fernández de Gurmendi, amesema kuwa Mahakama hiyo haiwaonei viongozi wa bara la Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza akiwa ziarani Kaskazini mwa Uganda, Jaji Fernández amesisitiza kuwa Mahakama hiyo lengo lake kuu ni kuhakikisha haki inatendeka kote duniani.

Ametoa wito pia kwa mataifa ya bara Afrika kama Burundi ambayo yamesema yatajiondoa katika Mahakama hiyo, kutofanya hivyo.

Mahakama nchini Afrika Kusini imeizua serikali kujiondoa huku rais mpya wa Gambia Adama Barrow akisema nchi yake haitajitoa katika Mahakama hiyo.