Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Felix Tshisekedi ateuliwa kuwa kiongozi wa Upinzani DRC, muwindaji wa Tanzania ahukumiwa miaka 12 jela

Sauti 21:03
Felix Tshisekedi, mtoto wa kinara wa Upinzani nchini DRC, desemba 21 2016.
Felix Tshisekedi, mtoto wa kinara wa Upinzani nchini DRC, desemba 21 2016. REUTERS/Thomas Mukoya

Makala hii imeangazia hatua ya muungano wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya kumteua Felix Tshisekedi kuwa kiongozi mpya wa muungano huo, baada ya kifo cha aliyekuwa kiongozi wa muungano huo, Etienne Tshisekedi jijini Brussels, Ubelgiji, pia muwindaji haramu wa pembe za ndovu nchini Tanzania ambaye pia alifahamika kama shetani wa wanyama amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela.lakini pia mgomo wa madaktari nchini Kenya, wakati katika uga wa kimataifa tumegusia siasa za Marekani, Ufaransa na kwingineko duniani.