Niger yatangaza hali ya tahadhari kufuatia tishio la mashambulizi ya wanajihadi
Imechapishwa:
Serikali ya Niger imetangaza hali ya tahadhari katika baadhi y amajimbo magharibi mwa maeneo yanayopakana na Mali baada ya mashambulizi kadhaa yanayodaiwa kutekelezwa na wanajihadi kutoka taifa jirani.
Taarifa ya serikali kupitia televisheni ya taifa hilo imearifiwa kutekelezwa katika idara saba za kiserikali za mikoa ya Tillaberi na Tahoua.
Vikosi vya ulinzi na usalama vimepewa nguvu na mamlaka zaidi ikiwemo haki ya kupekua makazi ya watu wakati wowote,ilieleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa serikali kujirudia kwa mashambulizi katika maeneo hayo kumehatarisha amani na kusababisha hofu miongoni mwa raia.
Maeneo yaliyoathirika ni "Ouallam, Ayorou, Bankilare, Abala na Banibangou katika mkoa wa Tillaberi na Tassara Tilia na Tahoua".