GAMBIA-BARROW-ULINZI

Askari waliojaribu kumpindua Jammeh warejeshwa kazini

Rais Adama Barrow wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika makaazi yake mjini Banjul, Januari 28, 2017.
Rais Adama Barrow wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika makaazi yake mjini Banjul, Januari 28, 2017. REUTERS/Thierry Gouegnon

Rais wa Gambia Adama Barrow ameamuru kurejeshwa katika jeshi askari sita walikua na hatia ya kuandaa mapinduzi dhidi ya mtangulizi wake Yahya Jammeh, chanzo cha kijeshi kimearifu.

Matangazo ya kibiashara

"Uongozi wa ukishauriana na Rais Adama Barrow, umeamua kuwarejesha katika jeshi la taifa Luteni Buba Sanneh, Modou Njie, Luteni Sarjo Jarju, Abdoulie Jobe Kapteni, Luteni Amadou Sowe na Buba Bojang " , chanzo hicho kimeliambia shirika la habari la AFP.

Aliyekua rais wa Gambia Yahya alisababisha majaribio kadhaa ya mapinduzi wakati wa utawala wake uliodumu miaka 22, jaribio mbaya la mapinduzi ni lile la mwaka 2,014. Askari walijaribu kuchukua udhibiti wa ikulu ya rais wakati alipokuwa nje ya nchi.

Askari watatu walikua walihukumia adhabu ya kifo

Askari hao sitawalikua walihukumiwa na mahakama ya kijeshi mwezi Aprili mwaka 2015, ikiwa ni pamoja na watatu ambao walihukumiwa adhabu ya kifo, lakini wafungwa hao walipewa msamaha na Rais Adama Barrow mwezi uliopita. Askari hao sita tayari wamejiunga tena na jeshi la taifa.

Desemba 30, 2014, kundi la watu waliojihami na silaha za kivita walishambulia Ikulu ya rais katika mji Banjul lakini walirejeshwa nyuma na vikosi vya yahya Jammeh.

Wiki moja baada ya kutambua matokeo ya uchaguzi wa rais mwezi Desemba mwaka jana, Yahya Jammeh alikataa kukabidhi madaraka kwa Adama Barrow. Aliondoka Gambia Januari 21 na kupelekwa uhamishoni nchini Equatorial Guinea baada ya kukabiliwa na shinikizo za kidiplomasia na kijeshi.