DRC

Polisi wa DRC waua wanamgambo wanne wa BDK

Polisi na wanamgambo watatu wameuawa wakati wa operesheni ya polisi ambayo ilimalizika siku ya Ijumaa kwa kujisalimisha kwa naibu, wa madhehebu ya dini na kisiasa, guru anayetajwa kwa kusababisha uasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mujibu wa ripoti rasmi iliyochapishwa jana Jumamosi. 

Wanajeshi wa jeshi la DRC
Wanajeshi wa jeshi la DRC Reuters
Matangazo ya kibiashara

Polisi ilitangaza Ijumaa jioni kujisalimisha kwa Ne Muanda Nsemi, kiongozi wa kiroho wa Bundu Dia Kongo (BDK), baada ya masaa kadhaa ya mapigano kati ya maafisa wa polisi na watu waliokuwa katika makazi yake katika kitongoji cha kaskazini mwa Kinshasa.

Wizara ya mawasiliano imesema katika taarifa kuwa operesheni ya polisi imefanikiwa kuwaua wanamgambo watatu wa BDK

Mwishoni mwa operesheni hiyo watu 307 walijisalimisha polisi lakini Muanda Nsemi, wake zake watatu na mtoto wake walifikishwa mbele ya mwendesha mashitaka ya umma kujibu makosa yao.

Kwa mujibu wa waraka huo, Ne Muanda Nsemi ni mshitakiwa miongoni mwa wengine kwa kosa dhidi ya mkuu wa nchi, uchochezi wa chuki ya kikabila, uchochezi kwa uasi wa raia, hata hivyo tarehe ya kesi yake haikuwekwa wazi.