MOROCCO-USALAMA

Mbunge auawa mbele ya nyumbani kwake

Marehemu "alipigwa risasi tatu za bunduki inayotumiwa kwa kuwinda wanyama,"  DGNS imesema.
Marehemu "alipigwa risasi tatu za bunduki inayotumiwa kwa kuwinda wanyama," DGNS imesema. Getty Images

Mtu mmoja anayehusika katika mauaji ya mbunge nchini Morocco amekamatwa siku moja baa ya mbunge huyo kuuawa kwa kupigwa risasi Jumanne wiki hii mbele ya nyumbani kwake.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka Kurugenzi ya Usalama wa Taifa (DGSN) Abdellatif Merdas, mwenye umri wa miaka 53, aliuawa Jumanne jioni mbele ya nyumbani kwake.

Polisi walikuta "mwili ndani ya gari yake mwenyewe."

Mbunge huyo alipigwa risasi tatu za bunduki inayotumiwa kwa kuwinda wanyama," DGNS imesema.

Bw Merdas alikuwa mbunge wa chama cha Umoja wa Katiba (UC) katika mkoa wa Ben Ahmedkilomita sitini kusini-mashariki mwa mji wa Casablanca.

Mtuhumiwa akamatwa

Kwa mujibu wa polisi, vielelezo ya kwanza vya uchunguzi vimepelekea "kukusanywa kwa ushahidi wa madai ya kuhusika kwa mtu binafsi kutoka mji wa Ben Ahmed kwa uhalifu a mauaji."

Mtuhumiwa, mwenye umri wa miaka 27, ana kesi nyingi mahakamani, na alikuwa alimtishiwa mbunge huyo baada ya kuibuka migogoro baina yao."

Mtuhumiwa alikamatwa nyumbani kwake katika mkoa wa Ben Ahmed, ambapo msako ulipelekea "kukamatwa kwa silaha mbili zinazotumiwa kwa kuwinda wanyama na risasi zinazofanana na zile zilizotumiwa kwa mauaji ya mbunge huyo.