AFRIKA KUSINI-WINNIE-AFYA

Aliyekuwa mke wa Mandela alazwa hospitalini Johannesburg

Winnie Mandela, aliye kuwa mke wa Nelson Mandela Madiba, hapa ni Oktoba 30 mwaka 2014, akikataliwa kupewa umiliki wa makazi ya Qunu.
Winnie Mandela, aliye kuwa mke wa Nelson Mandela Madiba, hapa ni Oktoba 30 mwaka 2014, akikataliwa kupewa umiliki wa makazi ya Qunu. AFP PHOTO/GIANLUIGI GUERCIA

Mjane wa aliyekua rais wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini Nelson Mandela Madiba, Winnie Madikizela-Mandela, amelazwa hospitalini kwa sababu za uchunguzi wa kiafya.

Matangazo ya kibiashara

Winnie Madikizela-Mandela ni mmoja kati ya mashujaa waliopinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Msemaji wake Victor Dlamini, ameviambia vyombo vya habari kuwa Bi Madikizela-Mandela alikuwa ameenda kufanyiwa uchunguzi wa kawaida lakini madaktari wakaamua alazwe.

Mwezi Disemba mwaka uliopita, Bi Madikizela-Mandela alilazwa hospitali hiyo lakini sababu za kulazwa kwake hospitalini haikutajwa.

Winnie Madikizela-Mandela amepelekwa katika hospitali ya Milpark mjini Johannesburg, kwa mujibu wa chanzo cha kifamilia.

Bi Madikizela-Mandela alikuwa mke wa Nelson Mandela, na alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi kusajiliwa kama mhudumu wa kijamii nchini Afrika Kusini.

Itafahamika kwamba hivi karibuni Winnie Madikizela-Mandela alikosoa vikali uongozi wa chama tawala cha taifa hilo ANC.