MOROCCO

Mahakama ya Morocco ya muhukumu kifungo jela raia wa Ufaransa kwa kufadhili ugaidi

Baadhi ya wapiganaji wa kijihadi.
Baadhi ya wapiganaji wa kijihadi. ZUMA PRESS/MAXPPP

Mahakama nchini Morocco imemuhuku kifungo cha miaka 4 jela raia mmoja wa Ufaransa, baada ya kumkuta na hatia ya kosa la kufadhili makundi ya kigaidi, keso ambayo imewashtua watetezi wa haki za binadamu.

Matangazo ya kibiashara

Raia huyo Thomas Gallay, mwenye umri wa miaka 36 anayefanya kazi kama injinia, alizuiliwa mwezi Februari mwaka 2016 kwenye hoteli moja ya kitalii ya Essaouira kwenye pwani ya Morocco.

Awali alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela, lakini kifungo hichi kilipungwa na mahakama ya rufaa ya Sale mjini Rabat.

Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu ikiwemo Amnesty International na Human Rights Watch, mwezi Novemba mwaka jana walieleza hofu yao kuhusu mwenendo wa kesi hiyo kwa kile walichosema ushahidi uliotolewa mahakamani ulikuwa unategemea mashahidi wa uongo.

"Nchini Morocco hata kama polisi watakuzuia kusoma ushahidi wako au kwa lugha yoyote ile usiyoielewa, ukishatia saini tu, basi ndio inakuwa tiketi yako ya kwenda jela", amesema Sarah Leah Whitson, mkurugenzi wa Human Rights Watch kwa nchi za mashariki ya kati na Afrika Kaskazini.

Kwa mujibu wa mama wa raia huyo wa Ufaransa, Beatrice Gallay, amesema mwanae alituhumiwa kwa kutoa kiasi cha Euro 74 kwa ndugu yake aliyekuwa anahusishwa kwenye kesi hiyo.

Mama huyo amesema mwanawe, amehukumiwa kwa kuzingatia ushahidi wa uongo ambao alitakiwa kuutoa na polisi ambao walimpa ushahidi wao ukiwa kwa maandishi ya kiarabu hata kama kwa wakati huo hakuelewa chochote.