NIGER_AMADOU-HAKI-SIASA

Kiongozi wa upinzani Niger ahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela

Hama Amadou, wakati huo alipokuwa Spika wa Bunge la Niger, Novemba 6, 2013 mjini  Niamey.
Hama Amadou, wakati huo alipokuwa Spika wa Bunge la Niger, Novemba 6, 2013 mjini Niamey. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Mwanasiasa mkuu wa upinzani nchini Niger, Hama Amadou, aliyechuku nafasi ya pili katika uchaguzi wa urais 2016, alihukumiwa Jumatatu hadi kifungo cha mwaka mmoja jela na Mahakama ya Rufaa ya mjini Niamey kwa kushiriki katika biashara ya watoto.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo wanasheria wake wanasema wataendelea kupambana hadi kosa hilo dhidi ya mteja wao lifutwe.

Hama Amadou ambaye anaishi kwa sasa nchini Ufaransa kwa karibu mwaka mmoja, hakuhudhuria kesi yake. Alishtakiwa kwa kosa la "kushiriki " kabla mashitaka yake kubadilishwa kwa kosa la "biashara ya watoto," kulingana na uamuzi wa jaji.

Itafahamika kwamba Bw Amadou alifungwa jela miezi minne aliporejea nchini akitokea uhamishoni mwezi Novemba 14, 2015, lakini alisafirishwa haraka nchini Ufaransa kwa sababu za kiafya Machi 16, 2016, ambako alitibiwa katika hospitali ya Marekani ya Neuilly-sur-Seine siku chache kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais, uchaguzi ambao alishinda rais anayemaliza muda wake Mahamadou Issoufou.

"Kuna utaratibu mwengine ambao tutatumia" Wakili Mossi Boubacar, mwanasheria wa Hama Amadou amesema.

Kesi ya siku moja

Kesi hiyo ambayo ilifunguliwa Jumatatu asubuhi ilidumu siku moja, wakati ambapo wanasheria wake walikua walisimamisha kushiriki kwenye kesi hiyo, wakisema kuwa taratibuza kuitishwa Hama Amadoumahakamani hazikuheshimishwa. Washtakiwa, wenyewe, hawakujibu maswali.

"Hama Amadou anaishi Ufaransa, kwa hiyo anapaswa kutumiwa nakala zake za mahakama nchini Ufaransa (...) lakini hakimu amebaini kwamba itabidi kuchunguza kwa kina ombi hili la ubatili ," ameshtumu Ali Kadri, mmoja wa wanasheria washitakiwa.