LIBYA-USALAMA

Vikosi vinavyomtii Haftar vyatangaza kuyateka maeneo 2 ya mafuta nchini Libya

Eneo la Mafuta la Ras Lanuf nchini Libya, Januari 11, 2017.
Eneo la Mafuta la Ras Lanuf nchini Libya, Januari 11, 2017. AFP

Majeshi yanayomtii Marshal Khalifa Haftar, kigogo mwenye nguvu mashariki mwa Libya, Jumanne wiki hii iyametangaza kuyateka maeneo mawili ya mafuta kutoka mikononi mwa makundi hasimu ya waasi.

Matangazo ya kibiashara

"Majeshi yamekomboa maeneo yote makubwa ya mafuta", katika mkoa wa kaskazini mwa Libya, amesema Khalifa al-Abidi, msemaji wa vikosi vinavyomtii Khalifa Haftar. Mkuu wa kikosi cha ulinzi kwenye maeneo hayo ya mafuta amethibitisha kutekwa kwa maeneo ya Ras Lanuf na al-Sedra.

Vikosi vya Libya vyatangaza kudhibiti robo ya mji wa Benghazi

Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu vikosi vya mashariki mwa Libya vilitangaza kudhibiti karibu eneo nzima lililokua likikabiliwa na mapambano ya muda mrefu katika mji wa Benghazi.

Nchi ya Libya inakabiliwa na mapigano kati ya majeshi ya serikali ya Umoja inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa na makundi ya waasi, ikiwa ni pamoja na vikosi vinavyomtii Marshal Khalifa Haftar.