ETHIOPIA-USALAMA

Idadi ya waliopoteza maisha yafikia 113 Addis Ababa

Mlima mkubwa wa taka nchini Ethiopia, nje kidogo ya mji wa Addis Ababa, Machi 12, 2017.
Mlima mkubwa wa taka nchini Ethiopia, nje kidogo ya mji wa Addis Ababa, Machi 12, 2017. AFP

Maporomoko ya taka yaliyotokea miwishoni mwa juma lililopita katika kitongoji cha mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa yamesababisha vifo vya watu 113, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na serikaliambayo imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo ilitokea Jumamosi usiku katika kijiji cha Reppi, ambapo taka za wakaazi wa mji wa Addis Ababa kwa nusu karne katika mazingira machafu na ambapo mamia ya watu wanaishi kwa kuokota chakula na vyuma.

"Jumla ya vifo vimefikiwa 113, ikiwa ni pamoja na wanaume 38 na wanawake 75," Dagmawit Moges, msemaji wa manispaa amesema. "Utafiti unaendelea naidadi ya vifo inaweza kuongezeka," ameongeza.

"Kwa uchache watu 80 hawajulikani walipo," alisema mkaazi wa kiji hicho. "Tunadhani tutaweza kupata miili yao iliyofukiwa huko," ameongeza.

Maporomoko ya taka yaliharibu nyumba kadhaa.