Maelfu ya raia waokolewa kutoka mikononi mwa Boko Haram
Imechapishwa:
Serikali ya Cameroon imetangaza kuwa zaidi ya watu 5,000 wameokolewa kutoka mikononi mwa kundi la Boko Haram, linaloendesha harakati zake za kigaidi katika baadhi ya chi za Afrika Magharibi.
Mateka hao, wengi wao ni wanawake, watoto na wazee.
Walikua wakizuiliwa katika moja ya kambi za kundi la Boko Haram.
Kambi walio kuwemo iliteketezwa, Waziri wa Habari wa Cameroon, Issa Tchiroma Bakary, amesema katika mkutano na waandishi wa habari.
Kwa Waziri wa Habari wa Cameroon, watu hao waliokolewa wameafirishwa katika kambi ya wakimbizi ilioko mjini Banki, nchini Nigeria, ambako wanapata matibabu.
Operesheni dhidi ya Boko Haram
Angalau wanamgamo 60 wenye msimamo mkali wameuawa na askari wa Cameroon na Nigeria katika operesheni kabambe ya kijeshi iliyoendeshwa tangu mwishoni mwa mwezi Januari.
Kundi la Boko Haram lilianzisha harakati zake za kigaidi tangu miaka saba iliyopita.Uasi huo wa Boko Haram umegharibu maisha ya zaidi ya watu 200,000 na zaidi ya watu milioni 5 kuyahama makazi yao.