SOMALIA-ULAYA-UHARAMIA-USALAMA

Meli yatekwa nyara nchini Somalia: Eunavfor yathibitisha kitendo cha uharamia

Aris 13, Meli iliyotekwa nyara katika pwani ya Puntland
Aris 13, Meli iliyotekwa nyara katika pwani ya Puntland Eunavfor

Meli iliyotekwa nyara Jumatatu, Machi 13 katika pwani ya Somalia ilikumbwa na kitendo chacha uharamia na watu wenye silaha ambao walichukua udhibiti wa meli kwa kuomba kudai fidia.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo lilitolewa Jumanne na kikosi cha majini cha Ulaya kinachopambana dhidi ya uharamia. Hatima ya wafanyakazi wa Meli na meli yenyewe kwa sasa imesimamishwa wakati mazungumzo yakiendelea.

Baadaye katika siku ya Jumanne mchana , saa 24 baada ya kukubaliwa, Mkuu wa kikosi cha majini cha Ulaya (Eunavfor) hatimaye ialiweza kuwasiliana kwa njia ya simu na nahodha wa Aris-13 iliyotekwa nyara. Nahodha huyo alithibitisha kwamba alikamatwa siku moja kabla na maharamia, na maharamia hawa wanaomba fidia ili meli iweze kuachiwa.

Wakati huo huo, serikali inayojitegemea ya Puntland ilitangaza kwamba alikuwa ilituma askari katika bandari ya Alula ambapo maeli hiyo imeedeshwa. Ni kijiji cha wavuvi kinachopatikana katika pwani ya kaskazini ya Somalia. Vikosi vya baharini vya Ulaya vinafuatilia kwa karibu meli hiyo vikiwa angani. Hali nilikua tulivu siku ya Jumanne.

Kwa mujibu wa wataalamu kadhaa, Aris-13 ililengwa kwa urahisi kutokana na kuzidiwa na mzigo wa mafuta inayobeba katika mji wa Djibouti, ilikuwa ikiendeshwa polepole na karibu na pwani ya Somalia.

Mazungumzo yanatazamiwa kuanza

Kwa maoni ya mtaalam, kuna uwezekano mazungumzo sasa yaanze kati ya kiongozi wa maharamia kwa upande mmoja, wafanyabiashara mahiri na kampuni ya bima ya meli kwa upande mwengine. Mazungumzo ambayo yanaweza kuchukua wiki kadhaa.

Baada ya utulivu, huu ni utekaji nyara wa kwanza na maharamia wa Somalia tangu mwaka 2012. Somalia ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anafanya ziara ya kikazi ya kushtukiza Jumatano wiki hii. Ziara hiyo haikutangazwa kwa sababu za kiusalama. Boris Johnson amekutana na rais mpya wa Somalia.