DRC-PAPA-UHUSIANO

Papa Francis afuta ziara yake DRC

Papa Francis alitembelea Parokia ya Sainte-Madeleine-de-Canossa, nje kidogo ya kaskazini mwa mji mkuu wa Italia Machi 12, 2017.
Papa Francis alitembelea Parokia ya Sainte-Madeleine-de-Canossa, nje kidogo ya kaskazini mwa mji mkuu wa Italia Machi 12, 2017. RUETERS/Alessandro Bianchi

Papa Francis hatozuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kiongozi wa Kanisa Katoliki mwenyewe ambaye alitangaza katika mahojiano wiki iliyopita na gazeti la kila wili la Ujerumani la Die Zeit.

Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo ilikuwa katika ratiba ya Papa Francis, lakini mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini DRC na uhusiano mbaya kati ya Kanisa nau tawala wa Rais Kabila umesababisha Papa Francis kufuta ziara yake nchini humo.

Sio siri tena, mahusiano kati ya Papa Francis na Joseph Kabila yanalegalega. Wakati ambapo rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alipopokelewa mjini Vatican mwezi Septemba uliyopita, Papa hakuja kumsalimu mgeni wake katika maktaba, ambapo kawaida kufanyikia mahojiano.

Siku kadhaa zilizopita, katika mahojiano na gazeti la kila wiki la Die Zeit, Papa Francis alisema kuwa asingeweza kuzuru mji wa Kinshasa, safari ambayo ilikua ikiandaliwa. "Ilikua ilipangiliwa kuwa Papa Francis angelizuru Congo zote mbili, laikini pamoja Kabila hali si nzuri, sidhani kama naweza kwenda," alisema Papa akihojiwa na gazeti la Ujerumani, na hivyo kufuta matumaini ya wananchi wengi wa DRC.

Ziara hizo ingelifanyika kati ya miezi ya Julai na Agosti, lakini hakuna ujumbe wowote kutoka Vatican ambayo umetumwa mjini Kinshasa kuandaa ziara ya Papa Francis.