ZIMBABWE-MAWARIRE-SIASA-HAKI

Kesi ya mpinzani mkuu wa Robert Mugabe, kufunguliwa Alhamisi hii

Kesi ya mchungaji Evan Mawarire, mpinzani mkuu wa Rais Robert Mugabe, imefunguliwa Alhamisi hii Machi 16 mjini Harare, nchini Zimbabwe. Katika nchi hii inayokabiliwa na mdororo wa kiuchumi, serikali imekua ikipiga marufuku maandamano yoyote ya upinzani.

Mchungaji Evan Mawarire akirikodi ujumbe wa video baada ya kuripoti mahakamani Februari 17, 2017 mjini Harare.
Mchungaji Evan Mawarire akirikodi ujumbe wa video baada ya kuripoti mahakamani Februari 17, 2017 mjini Harare. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Baada ya serikali kujaribu kumdhibiti, Evan Mawarire hatimaye amekua maarufu nchini Zimbabwe. Raia wengi wanatazamiwa kukusanyika mbele ya mahakam muda wowot kesi hiyo itakua ikisikilizwa.

Mwezi Februari Mchungaji Mawarire alifaulu kufika kwenye uwanja wa ndege wa mjini lakini wakati huo huo alikamatwa na polisi. Alikua akirudi nyumbani akitokea uhamishoni ambapo aliishi miezi sita nchini Afrika Kusini, ambako alikimbilia baada ya kuzuiliwa jela kwa siku chache.

Mchungaji Evan Mawarire hakua anajulikana kisiasa mwaka mmoja uliyopita, lakini kwa sasani mtu maarufu na kiongozi wa upinzani dhidi ya Robert Mugabe.

Hata hivyo Mchungaji Mawarire alijikuta amekua mwanasiasa shupavu, kama alivyosema dadake, Telda. Evan Mawarire, mwenye umri wa miaka 39 hajajiunga na chama chochote cha kisiasa.

Mwezi Aprili 2016, alijiuliza jinsi ya kulipia masomo ya binti zake wawili nawakati huo huo alichukua uamuzi wa kupigwa picha na kurikodiwa sauti.

Katika video yake ya kwanza iliyowekwa hewani nchini Zimbabwe, Mchungaji Mwarire alionekana akivaa bendera ya Zimbabwe shingoni mwake, hukua akishtumu utawala wa Robert Mugabe kujihusisha na rushwa na kusababisha hali ngumu ya maisha kwa wananchi wake. Mara baada ya video hiyo kurushwa hewani, mamia kwa maelfu ya raia walimiminika mitaani wakiandamana wakipinga hali ngumu ya maisha inayowakabili.

Rais Robert Mugabe anatawala nchi ya Zimbabwe kwa miaka 37 sasa.