Rais mpya wa CAF kuchaguliwa Alhamisi hii
Imechapishwa:
Uchaguzi mkuu wa rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) unafanyika Alhamisi hii Machi 16 katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia. Issa Hayatou, rais wa shirikisho hilo anayemaliza muda wake anachuana na Ahmad Ahmad, rais wa chama cha Soka nchini Madagascar.
Issa Hayatou kutoka Cameroon, anatetea nafasi yake anayoishikilia toka mwaka 1988.
siku ya Jumatano mshindani wa Issa hayatou, Ahmad Ahmad, alikua akihamasisha na kuwashawishi marais wa vyama vya soka kutoka nchi mbalimbali mjini Addis Ababa kumpigia kura. Bw Ahmad ameendelea kuamini kwamba anaweza kumuangusha Issa Hayatou Cameroon.
Itafahamika kwamba Ahmad Ahmad hakuhudhuria filamu ya miaka 60 ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Duru za kuaminika zinasema kuwa, kumekua kukifanyika mazungumzo ya chini kwa chini kuhusu uchaguzi wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji, uchaguzi wa wawakilishi wa Afrika kwenye Baraza la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na uchaguzi rais mpya wa CAF.
"Sawa, mambo yanakwenda vizuri, " amesema Ahmad kuhusukuwania kwake, kabla ya kwenda kufanya kukutana na wale wanaomuunga mkono.
All set for the 39th CAF Gneral Assembly - Addis ababa 2017 pic.twitter.com/xoJsldqWDX
— CAF (@CAF_Online) March 16, 2017