Mazungumzo yaanza katika hali ya mvutano DRC
Mazungumzo kati ya wanasiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yameanza tangu Alhamisi wiki hii wakati ambapo mvutano wa kisiasa bado unaendelea.
Imechapishwa:
yama vinavyounga mkono serikali, upinzani na mashrika ya kiraia walikutana Alhamisi hii na Baraza Kuu la Maaskofu wa kanisa Katoliki (Cenco) kwa lengo la kuendelea na mazungumzo mabyo yalikua yalisimama kwa siku kadhaa, tangu mwishoni mwa mwezi Januari.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Baraza Kuu la Maaskofu wa kanisa Katoliki ufunguzi kikao cha mwisho cha mazungumzo kati ya wadau wote nchini DRC kilifanyika mwishoni mwa mwezi Januari.
Licha ya mazungumzo hayo kuanza Alhamisi, hali ya kutoelewana imeshuhudiwa baada ya kikao hicho cha mazungumzo ya Alhamisi. Jambo ambalo lilimkasirikisha Naibu Mwenyekiti wa Cenco, Askofu Fridolin Ambongo.
Miongoni mwa masuala yaliyozungumziwa, ni pamoja na mfumo wa uteuzi wa Waziri Mkuu. Vyama vinavyounga mkono serikali vinaoa kwamba kuna haja ya kupendekezwa majina ya watu watatu kwa Rais Kabila, lakini muungano wa upinzani wa Rassemblement unaona kuwa jina moja peke linatosha.