SOMALIA-SRILANKA-USALAMA

Meli iliyokua ikishikiliwa na maharamia wa Somalia yaachiwa

«Aris 13», katika pwani ya Puntland.
«Aris 13», katika pwani ya Puntland. Eunavfor

Kikosi cha majini cha Ulaya kinachopambana na uharamia kimethibitisha kuwa maharamia wameamua kuiachilia "Aris 13", meli ya Sri Lanka iliyokua ikibeba mafuta ambayo ilikua ikishikiliwa na maharamia hao tangu mwanzoni mwa wiki hii. Wafanyakazi wa meli hiyo wako salama, kwa mujubu wa kikosi hicho.

Matangazo ya kibiashara

"Aris 13" ilikua imebeba mafuta na gesi kutoka Djibouti kuelekea Mogadishu wakati ilishambuliwa Jumatatu na watu wenye silaha katika meli mbili.

"Kikosi cha walinzi katika pwani ya Puntland, waliwataka maharamia kuiachia meli hiyo bila masharti, jambo amblo lilifanyika bila upinzani wowote, " John Steed, afisa wa shirika lisilo la kiserikali la Oceans Beyond Piracy (OPB) linalopambana dhidi ya uharamia ameliambia shirika la habari la AFP.

Maharamia wa Kisomali waliitka meli hiyo ya mafuta Aris 13 Jumatatu wiki hii, shambulio la kwanza lililofaulu la meli ya kibiashara katika pwani ya Somalia tangu mwaka 2012.

Kikosi cha majini cha Ulaya dhidi ya uharamia kilisema Jumanne wiki hii kwamba kiliwasiliana na nahodha wa meli hiyo, ambaye aliwaambia kuwa maharamia wanadai fidia.

Siku ya Alhamisi, kikosi cha walinzi katika pwani ya Puntland kimewatishia maharamia kukabiliana na kama wakataa kuiachia meli hiyo na wafanyakazi wake.